Kendall Jenner hafurahii mahusiano ya Tyga na Kyle

Dada wa mwanamitindo Kyle Jenner ambaye pia ni mwanafamilia wa Kardashian Kendall Jenner, ameoneshwa kutofurahishwa na mahusiano ya kimapenzi ya mdogo wake Kyle na mwanamuziki maarufu Tyga.

Kendal Jener ameoneshwa kutofurahia mahusiano hayo baada ya kusema kuwa Tyga alitakiwa kuwa nyumbani na familia yake, kwa wakati ambao aliungana na familia ya Kardashian katika siku maalum ya mapumziko na familia ambapo familia hiyo ilienda kupumzika St. Barts.

Kwenye mfululizo wa kipindi chao cha Keeping up with the Kardashian dada yao mkubwa Kim Kardashian ambaye ni mke wa mwanamuziki maarufu duniani Kanye West, alisikika akiwataarifu kuwa Kyle anamleta Tyga kwenye safari yao, ndipo Kendal alipotoa maneno hayo.

“Ungechukua muda huu kuwa na familia yako”, alisema Kendal ambaye alikuwa anamwambia Kyle juu ya mpenzi wake Tyga.

Kyle na Tyga wameanza mahusiano yao mara baada ya Tyga kuachana na mpenzi wake Black Chyna, ambaye pia ni mama wa mtoto wake mmoja King, na kuibua minong’ono mingi kwa watu kuwa Kyle ndio chanzo cha kuachana na mama wa mtoto wake.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s