Mwanafunzi UDSM auawa kwa risasi

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Mutaengerwa Mafwiri ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi jana usiku eneo la Msewe jijini Dar es Salaam.

mwanafunzi

Akizungumza na http://www.globalpublishers.co.tz kwa njia ya simu, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Camillus Wambura amekiri kutokea kwa tukio hilo.

Kwa mujibu wa Kamanda Wambura tukio hilo lilitokea jana usiku majira ya saa mbili baada ya watu wanaosadikiwa kuwa majambazi kuvamia duka moja lililopo maeneo hayo na kupora simu, vocha na fedha taslimu kiasi cha shilingi 100,000/=.

Wakati wakiondoka eneo la tukio wananchi walianza kuwapigia kelele ndipo walipoanza kupiga risasi ovyo ambapo mojawapo ilimpata Mafwiri aliyekuwa katika banda la chipsi na kumsababishia umauti.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na uchunguzi bado unaendelea.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s