Barnaba: Sauti yangu inawafanya wanisikilize nikiimba

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Elias Barnaba a.k.a Barnaba Boy Classic amesema kwamba sauti aliyonayo ndiyo inamfanya aonekane kuwa msanii mzuri, pamoja na mwenendo mzuri mbele ya jamii.

 Barnaba ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano katika kipindi cha 5SELEKT kinachorushwa na East Africa Television , na kuelezea sifa hiyo ya pekee ambayo anayo.

”Mimi nikiimba hata kama hujaniona na niko nyuma ya ukuta ukisikia sauti inavotoka tuu lazima utatoka kuja kusikiliza na kuungana na mimi” alisema Barnaba.

Akiongelea kazi zake za muziki Barnaba amesema ana kazi nyingi ambazo ameshazikamilisha, lakini anaangalia ubora wake kwanza kabla hajaziachia.

”Mimi nina ngoma nyingi sana ambazo naweza ziachia muda wowote lakini ni bora nitoe ngoma tano tuu ambazo zitakuwa zimepangiliwa vizuri sana kwa mwaka, ambazo zitakua na mashiko kuliko kutoa ngoma 15 ambazo zinakua hazifiki popote” alisema Barnaba

Aidha Barnaba amebainisha moyo wa kujituma kwa wasanii yeyote ndiyo nguzo itakayowawezesha kufika mbali, na kufanya vizuri katika muziki ndani na nje ya nchi.

Kuhusu suala la kusaidia wanamuziki chipukizi Barnaba amesema lebo ya High Table Sound itatoa kipaumbele kwa wasanii wa kike kwanza, hivyo ni vema wakatembelea ukurasa wake wa mitandano ya kijamii kupata maelekezo ya nini cha kufanya, na atawaita katika studio yake na kufanya nao kazi.

Hata hivyo amewashukuru Watanzania wote, vyombo vya habari, wanamuziki wenzake na watu wote ambao wamekuwa wakimshauri namna ya kuendeleza muziki wake, na amewaaahidi atafanya vizuri zaidi na atatoa ngoma kali na video za kimataifa, ambazo zitakuwa na manufaa katika muziki wetu.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s