Mchezaji aliyemtongoza mwanahabari aadhibiwa

Nahodha wa zamani wa timu ya kriketi ya West Indies, Chris Gayle amepigwa faini baada yake kumtongoza mwanahabari wakati wa mahojiano ya moja kwa moja.

 150215222149_chris_gayle_640x360_getty

Gayle amepigwa faini ya dola 10,000 za Australia (sawa na $7,200; £4,900) na klabu yake ya Melbourne Renegades inayocheza ligi ya Big Bash.

Mchezaji huyo alimuuliza mwanahabari wa kipindi cha Ten Sport Bi Mel McLaughlin kama wangeweza kwenda ‘date’ alipokuwa akihojiwa wakati wa mechi ya ligi dhidi ya Hobart Hurricanes Jumatatu.

“Kuyatazama macho yako mara ya kwanza kabisa ni jambo njema sana. Natumai tunaweza kuketi na kunywa kinywaji pamoja. Usione haya mtoto,” alimwambia.

Baadaye, amejitetea na kusema alikuwa tu anafanya mzaha.

Chris Rogers, aliyekuwa nahodha wa Sydney Thunder wakati Gayle alikuwa mchezaji wa kawaida ameambia shirika la habari la ABC Grandstand kwamba hajashangazwa na kitendo hicho cha Gayle.

Gayle

Klabu ya Melbourne Renegades imesema matamshi hayo yalikuwa hayafai kabisa na yalikuwa ya “kuvunja heshima”.

Maafisa wa klabu hiyo wameomba radhi kwa McLaughlin na umma pia.

Pesa kutoka kwa faini aliyotozwa mchezaji huyo zitakjabidhiwa wakfu wa McGrath unaosaidia watu wanaotatizwa na saratani ya matiti.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s