Zidane akabidhiwa mikoba ya Rafael Benitez

Uongozi wa klabu ya Real Madrid umememteua Zinedine Zidane Zizou kuwa kocha wa muda baada ya kufuta kazi kocha wake Rafael Benitez ambaye amedumumu Miezi saba tu katika Mkataba wake wa Miaka Mitatu.

<img src=”http://www.eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/news/2016/01/05/ZIDANE%202_1.jpg?itok=2pWXAgIZ” width=”630″ height=”453″ alt=”” />

kocha mpya wa Real Madrid Zinedine Zidane enzi zake za uchezaji akifanya tukio la kihistoria la kumpiga kichwa beki wa Italia Marco Materazzi kwenye fainali za kombe la dunia nchini Ujerumani.

Zidane ambae alitwaa Kombe la Dunia akiwa Mchezaji na Nchi yake ya Ufaransa Mwaka 1998, aliwahi kuwa Mchezaji wa Real kuanzia 2001 aliponunuliwa kwa Rekodi ya Dunia wakati huo kutoka Juventus na kucheza hadi 2006.

Zizou amekabidhiwa mikoba hiyo akitokea katika timu B kutokana na matokeo mabaya kwa timu hiyo, ambapo ilitoka Sare 2-2 na Valencia katika Mechi ya La Liga, Sare ambayo imewaacha Vigogo hao Nafasi ya tatu wakiwa nyuma ya Atletico Madrid kwa pointi 4.

Tangu atue Madrid Benitez amekuwa si kipenzi cha Mashabiki wa Klabu hiyo, baada ya kufungwa bao 4-0 kwenye mechi ya El Clasico Mwezi Novemba na Mahasimu wao Barcelona , Pia kutupwa nje ya michuano ya Copa del Rey.

Hali hiyo imefanya kuwepo minong’ono ya kila mara kuwa Wachezaji wa Real hawana raha na Benitez na wana mgomo baridi dhidi yake.
Wiki iliyopita Benitez aliwatuhumu Wanahabari kwa kuendesha kampeni kumpinga yeye, Klabu na Rais wao Florentino Peréz.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s