Serikali yawataka waishio mabondeni kutii sheria.

Watanzania wameombwa kuhama katika maeneo ya mabondeni haraka iwezekanavyo ili kupisha zoezi la bomoa bomoa ambalo linaendelea hivi sasa jijini Dar es salaam.

DSC_0226

Hayo yamezungumzwa na Mkurugenzi msaidizi wa usimamizi wa udhibiti na uhendeshaji miji wizara ya ardhi na maendeleo ya makazi, George Pangawe leo jijini Dar es salaam akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na zoezi linaloendelea la ubomoaji katika kingo za mto msimbazi.

Pangawe amesema kuwa zoezi la ubomoaji linaloendelea la ubomoaji ni katika kutekeleza mpango kabambe wa jiji la DSM wa mwaka 1979 ambao unaeleza kuwa bonde la msimbazi ni sehemu hatarishi kwa makazi ya binadamu.

DSC_0229
Baadhi ya waandishi wa habari ambao waliudhuria katika kikao, wakimsikiliza mkurugenzi msaidizi wa usimamizi na udhibiti wa uendeshaji miji wizara ya ardhi na maendeleo ya maakazi George Pangawe.

Amesema kuwa serikali itahakikisha haki ikitendeka kwa watu waishio katika bonde hilo katika pande zote, wakati wa utekelezaji wake ambao ulisimama December 22 na kuanza tena januari 5 mwaka huu.

Akiongeza kuhusu karakana ya mradi wa mabasi yaendayo kwa kasi (DART) amesema kuwa mradi huo umefuata sheria ya mazingira kifupi 57(2) inatoa nafasi ya kutolewa ruhusa kwa miradi/shughuli zenye maslahi kwa taifa kufanyika katika maeneo ya mabondeni, hivyo mradi huo ulipata kibali cha mazingira na unaendelea kutekeleza mpango wa usimamizi wa mazingira.

Mwisho amewapongeza wananchi ambao wamehama mapema na amewataka wananchi  wengine ambao wamesalia kufuata sheria ili kuepuka na adha mbalimbali ikiwamo upotevu wa mali zao kipindi cha zoezi hilo.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s