UTT yazindua “Pamoja Bima”

Mfuko wa UTT wakishirikiana na taasis za bima Jubilee insuarance  company na Britam Isurance wamezindua mfuko wa “Pamoja Bima” ambayo itakuwa ina husika kwa kina na bima za magari pamoja na bima ya masuala ya nyumbani.

DSCN0137

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam mkurugenzi wa jubilee George Alande amesema kuwa Bima hiyo itakuwa inahusiana na bima ya magari na mambo yote ya nyumba, ambapo bima hiyo kwa upande wa magari itahusian na upotevu au kuharibika kwa gari kutokana na wizi, moto na utatu.

Hata hivyo kwa upande wake mkurugenzi wa Britam Stephen Lokonyo ameongeza kuwa bima ya nyumba itakuwa inahusiana na makazi, na majanga yote yanayoweza kuikumba nyumba, ikiwamo nyumba kuungua moto, dhoruba, mafuriko matetemeko ya ardhi, huku kaya ikiwa inahusiana na wizi, upotevu wa vifaa ama vyombo vya ndani kama friji, Tv, radio na kadhalika.

DSCN0203

Wakati huo huo mkurugenzi wa UTT  Hamis Kibola amekubaliana moja kwa moja na “Pamoja Bima” kwa kusema kuwa mteja hatonufaika na faida za bima tu bali pia ata furahia faida za kuwekeza kwa kununua hisa katika nfuko wa Umoja. pia pamoja Bima itahamasisha kuwa na akiba miongoni mwa wateja.

UTT ni taasisi ya kifedha ambayo ilikuwa ikimilikiwa na serikali ya jamhuri wa muungano wa Tanzania ambayo ililetwa katika kutekeleza sera za serikali ambazo zilikuwa katika kuwawezesha watu wenye maisha ya wastani na ya chini tangu mwaka 2013 UTT imekuwa na kufikia matawi 10 nchini.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s