Japani yatoa bilioni 210 za mradi mkubwa wa umeme

Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la nchini Japan – JICA, limesaini makubaliano ya kuikopesha serikali shilingi bilioni 210 za ujenzi wa njia ya umeme utakaoziunganiisha Tanzania na Kenya

Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la nchini Japan – JICA, leo limesaini makubaliano na Wizara ya Fedha na Mipango ambapo lishirika hilo litaipatia serikali ya Tanzania mkopo wa shilingi bilioni 210 kwa ajili ya ujenzi wa kilomita 508 za njia ya umeme utakaoziunganisha Tanzania na Kenya.

Akizungumza mara baada ya kusaini makubaliano hayo, mwakilishi mkazi wa JICA nchini Bw. Toshio Nagase amesema Tanzania ndiyo itakayofaidika zaidi na fedha hizo kwani kati ya kilomita 508 za umeme zitakazojengwa, kilomita 415 zipo nchini Tanzania na 93 zilizobakia zipo nchini Kenya.

Kwa mujibu wa Bw. Nagase, mradi huo unatarajia kukamilika ifikapo mwaka 2019 na kwamba mara utakapokamilika, utachochea kasi ya ukuaji wa uchumi kwani Tanzania na Kenya zitakuwa na nishati ya uhakika kwa ajili ya uzalishaji mali.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s