Profesa Mbarawa atumbua majipu ya bandari awatimua vigogo.

WAZIRI wa Ujenzi,uchukuzi na mawasiliano,Profesa Makame Mbarawa amewahamisha kazi watendaji wa juu wa Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) baada kuisababishia serikali hasara kwenye upotevu wa makontena katika bandari hiyo.

Watendaji hao waliohamishwa kazi ni, Piter gawilo ambaye alikuwa mkurugenzi wa Rasilimali watu ndani ya Mamlaka hiyo,ambaye ameondolewa kwenye nafasi hiyo na nafasi yake kuchukuliwa na Antony Mbilinyi ambaye awali alikuwa mkurugenzi wa Rasilimali watu ndani ya Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA).

Wengine ni waliomishwa Kazi ni Kaimu mkurugenzi wa manunuzi wa TPA, Mashaka Kishanda ambaye nafasi yake nafasi yake imechukuliwa Benito Kalinga ambaye awali alikuwa mtumishi wizarani hapo,

Sanjari hao, mwengine aliohamishwa ni Kaimu mkurugenzi wa TEHEMA wa TPA,Kalian Charles naye nafasi yake imechuliwa Abdullhaman Bamba ambaye awali naye pia walikuwa wizarani ya ujenzi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam waziri Mbarawa amesema nia ya serikali ya kuwaondoa watendaji hao ni kukata kuongoza kasi ya ukusanyaji mapato ndani ya TPA.

“Serikali imefuikia uaamuzi huu,kwa lengo la kuongeza kasi ya ukusanyaji kodi kwenye Mamlaka ya Bandari ndio maana tumewaondoa watendaji hawa tumewaweka watu ambao watazidisha kasi ya ukusanyaji mapato “amesema Waziri Mbarawa.

Hata hivyo,Waziri Mbarawa amesema watendaji hao waliondolewa kwenye nafasi hizo,wamerejeshwa wizarani na kusubuli kupangiwa kazi nyengine.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s