Kisarawe Cements, “yatisha” kwa kuchangia mifuko 200 ya saruji.

Kampuni ya Kisarawe Cement inayotengeneza seruji ya Lucky cement leo wamekabidhi mifuko 200 ya saruji katika harakati za kumuunga mkono mkuu wa wilaya ya kinondoni, Paul Makonda kwa ajili ya ujenzi wa shule za sekondari.

 DSCN7711.JPG

Akikabidhi mifuko hiyo mapema leo katika ofisi za mkuu wa wilaya Bi. Florence Mashakangoto, mbele ya waandishi wa habari amesema kuwa, kampuni imeamua kumuunga mkono mheshimiwa Paul Makonda kwa kuhakikisha watanzania wanapata elimu ambayo itawawezesha watoto kufikia ndoto na malengo yao.

DSCN7731

“Tumeamua kutoa mchango wa wetu wa mifuko 200 katika kuhakikisha kampeni ya uboreshaji wa elimu katika manispaa ya kinondoni ambayo imeanzishwa na Mhesimiwa Makonda inafanikiwa kwa kuwa tunatambua umuhimu wa elimu, kwa watoto ambao wanaweza kuwa madaktari, waandishi au hata marais.”

 

Pia ameyataka makampuni mengine ambayo yanajishughulisha na utengenezaji wa saruji, mabati, Nondo na vifaa vingine vya ujenzi, kujitokeza kwa wingi katika kushiriki kuchangia zoezi hilo katika kutekeleza azma ya ujenzi wa shule za kata 7 zilizopo katika wilaya ya kinondoni.

 

Kwa upande wake mkuu wa wilaya hiyo Paul Makonda amewashukuru Luck Cement kwa kuuona umuhimu wa kusaidia kinondoni ambayo imetoa idadi ya shule nne(4) katika kumi bora ya katika mtihani wa kidato cha pili na hawajaingia kumi za mwisho kitaifa.

Makonda alianzisha kampeni hii ya uchangiaji wa ujenzi wa shule kata saba mwishoni mwa mwaka jana ili kupunguza tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa katika shule zote za kata na kuongeza idadi ya shule ambazo zinapatikana katika wilaya ya kinondoni.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s