NMB na John Deere wasiani makubaliano kusaidia wakulima

Kampuni maarufu kwa uuzaji wa matrekta duniani ya John Deere imeingia makubaliano na benki ya NMB ili kutoa mikopo nafuu kwa wakulima wanaochipukia nchini ili kurahisisha kupata vifaa vya kilimo.

12507468_826557914121312_128293008904951321_n

Akiingia makubaliano hayo mkurugenzi wa John Deere kwa nchi za kusini mwa jangwa la sahara Antois Van Der Westhuizen amesema kuwa mikopo hiyo ya matrekta itakayotolewa na NMB kwa kushirikiana na kampuni yake ina lengo la kuinua wakulima wadogo kubadilisha kilimo kutoka kilimo cha mazoea kuwa kilimo endelevu chenye kutumia vifaa vya kisasa kama matrekta ya kulimia, kuvunia na pia kusafirisha mazao.

12472244_826559217454515_1024534253615450856_n

Kwa  upande wake mkuu wa kitengo cha wateja wakubwa wa NMB Filbert Mponzi alisema kuwa benki inatambua umuhimu wa sekta ya kilimo katika ukuaji wa uchumi wa nchi na hivyo imechukua hatua madhubuti kuingia makubaliano na makampuni pia kubuni bidhaa zinazolenga  kuboresha sekta ya kilimo.

1916635_826516460792124_7133808802530815236_n

“NMB tumwafikia zaidi ya wakulima wadogo 600,000 kwa kusaidia mitaji kwaajili ya uzalishaji wa mazao ya kilimo, pia tunasaidia wakulima wakubwa ili waweze kukua zaidi. katika mipango ya benki ya uwajibikaji kwa jamii, tunatoa elimu kwa wajasiliamali kupitia mafunzo mbalimbali ya kibiashara na hivyo kuwawezesha kwa taarifa na uelewa jinsi ya kutunza fedha na pia kukuza mitaji.”

12523137_826559317454505_4945591205639029322_n

hata hivyo Mkurugenzi wa LonAgro Tanzania Lukas Botha alisema kuwa kupitia makubaliano kati ya NMB na John Deere, wakulima wana uhakika wa kupata nyenzo muhimu za kufanya ukulima kwa tekinolojia ya kisasa kuwezekana na wana uhakika wa kupata ushirikiano mkubwa kutoka LOnAgros na kufanya  ushirikiano endelevu.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s