Waliouza kiwanja Golden Tulip wasimamishwe: Lukuvi

Serikali imevunja uzio wa eneo la maegesho ya magari wa hoteli ya Golden Tulip Jijini Dar es salaam kutokana na umiliki wa eneo hilo kutolewa kwa njia zisizo halali.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya serikali kushinda kesi dhidi ya kampuni hiyo.

 

Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi nchini Tanzania William Lukuvi ameagiza kusimamishwa kazi wafanyakazi wote waliohusika kutoa hati na kuruhusu matumizi ya ardhi ya serikali katika kiwanja nambari 2048 kilichopo ufukweni Masaki Kinondoni jijini Dar es salaam.

Mh. Lukuvi ametoa agizo hilo leo jijini Dar es salaam wakati akishuhudia zoezi la bomobomoa katika kiwanja hicho kilichokuwa kimezungushiwa mabati ili kutaka kuliendeleza kinyume na sheria zoezi lililokuwa likitekelezwa na kampuni ya Indian Oceana Hotels Limited.

Katika agizo la Waziri Lukuvi ametaka baraza la usimamizi wa mazingira NEMC, Manispaa ya Kinondoni na ofisi yake kufanya kazi kwa pamoja kuwabaini wote waliohusika kutoa hati hizo.

Aidha Mh. Lukuvi amemwagiza katibu mkuu mara apatapo faili zenye majina hayo kupeleka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU.

eatv.tv

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s