CRDB yawaondoa wasiwasi Wateja wake.

Mkurugenzi wa benki ya CRDB Dr. Charles Kimei amewaondoa shaka wateja na wananchi kutokana na serikali kuchukua hatua za kupunguza riba za mabenki kwa wananchi kwa kuagiza akaunti za mashirika na taasisi zake katika mabenki ya biashara zifungwe na kuhamisha fedha zilizoko katika akaunti hizo kwenda akaunti zitakazofunguliwa Benki Kuu (BoT).

untitled 12

Akizungumza na waandishi wa habari leo Dr. Charles Kimei amesema kuwa hatua hiyo ya serikali wao kama CRDB wanaunga mkono agizo hilo lilotolewa na Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru hivi karibuni, akiwataka watendaji wakuu wote wa mashirika na taasisi hizo, kufuata maelekezo matano ya kufunga akaunti zao katika mabenki ya biashara na kuhamishia fedha hizo BoT.

“sisi kama CRDB tunaunga mkono moja kwa moja kwa kuwa serikali ina haki zote za kufanya hivyo kwa kuwa itasaidia serikali kugundua pesa zilizomo kwenye akaunti zake, hata hivyo kuna baadhi ya nchi tayari wameshatekeleza hatua kama hizo mfano Rwanda na Uganda,” alisema Dr. Kimei.

Kwahiyo kwa upande wa CRDB haitoathiri kitu chochote kama watafunga au kuhamisha fedha zilizoko katika akaunti hizo zitakazofunguliwa benki kuu (BoT), kwahiyo wananchi na wateja wetu wasiwe na shaka juu ya benki yao kila kitu kitakuwa vile vile kama awali na huduma zitaendelea kuboreshwa.

Akiongeza Dr. Kimei alisema hadi sasa ni karibia bilioni 500 shilling ambazo ziko katika mabenki ya biashar, na hatua hii haitoathiri pesa za kigeni kwa kuwa inahusu pesa ya wazawa (Shillingi) na pia kama serokali itaimarisha kutosafiri mara kwa mara pia shilling hitaimarika.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s