Rais Magufuli alaani kuuawa kwa Rubani Roger Gower

Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amelaani kitendo cha watu wanaosadikiwa kuwa ni majangili kumuua kwa kumpiga risasi Rubani wa helkopta Roger Gower, raia wa Uingereza na kisha kuidondosha helkopta aliyokuwa akiiendesha.

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Jumanne Maghembe akiwa eneo la tukio ilipotunguliwa helkopta ya TANAPA iliyomuua Kept. Roger Gower.

Tukio hilo limetokea wakati alipoungana na Askari wanyamapori waliokuwa wakikabiliana na majangili katika pori la akiba lililopo katika wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu.

Rais Magufuli ameelezea kusikitishwa sana na tukio hilo na ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kuhakikisha waliomuua Rubani Gower na kuidondosha helkopta aliyokuwa akiiendesha wanakamatwa na wanafikishwa mikononi mwa vyombo vya sheria.

Amemtumia salamu za pole, Balozi wa Uingereza hapa nchini kwa kumpoteza raia wake ambaye alikuwa akitoa mchango mkubwa katika kuhifadhi wanyamapori wa hapa nchini Tanzania.

Aidha, Rais Magufuli amesema serikali yake itahakikisha inaendeleza mapambano dhidi ya ujangili kwa nguvu zake zote na kuwataka wananchi na wadau mbalimbali wa hifadhi ya wanyamapori, kutokatishwa tamaa na tukio hili na watoe ushirikiano wa kutosha kuwafichua watu wote wanaojihusisha na ujangili ama biashara ya bidhaa zitokanazo na ujangili.

Katika tukio hilo, pamoja na kumuua Rubani Roger Gower watu hao wanaosadikiwa kuwa majangili wamemjeruhi Askari wanyama pori mmoja na wamewaua tembo watatu.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s