TRL yakabiliwa na ‘ukata’

Shirika la Reli nchini Tanzania – TRL lipo katika hali mbaya ya kiuchumi kutokana na ufanisi na mwenendo usioridhisha.

Shirika la Reli nchini Tanzania – TRL lipo katika hali mbaya ya kiuchumi kutokana na ufanisi na mwenendo usioridhisha, unaochangiwa na sababu mbali mbali mojawapo ikiwa ni tuhuma za ubadhirifu pamoja na matumizi ya zana na vifaa duni ambavyo haviendani na mahitaji ya sasa ya uendeshaji wa shirika hilo kibiashara.

 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Ujenzi na Uchukuzi Dkt. Leonard Chamuliho amekiri uwepo wa hali hiyo, wakati wa mkutano wake na wafanyakazi wa TRL, mkutano uliofanyika kwenye karakana ya makao makuu ya shirika hilo jijini Dar es salaam hii leo.

Kwa upande wake, Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli – TRAWU Bw. Shehe Shuhuli, ameitaka serikali kuharakisha uchunguzi wa sakata la ununuzi wa mabehewa yanayodaiwa kuwa chini ya kiwango; sambamba na kuendelea kuwalipa mishahara na stahili zote wafanyakazi zaidi ya elfu mbili wa shirika hilo kutokana na kushuka kwa ufanisi aliodai kuwa umechangiwa na serikali yenyewe.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s