Aliyetegua kitendawili cha Kanye West

Kijana mmoja nchini nchini Marekani anatarajia zawadi kutoka kwa mwanamuziki Kanye West baada yake kufanikiwa kujibu swali lake.

160212111222_dante_holley_512x288__nocredit

Dante Holley, 20, alifanikiwa kueleza kwa kirefu herufi TLOP zinasimamia nini kwenye jina la albamu ya mwanamuziki huyo ulio ambalo limetolewa kutoka kwa wimbo wake mpya kwa jina No More Parties in LA.

Atapokea tiketi za kuhudhuria maonyesho ya mavazi ya Kanye West ya Yeezy makala ya tatu, pamoja na mavazi yenyewe.

Iwapo bado unatafakari zinasimamia nini, zinasimamia The Life of Pablo.

“Alikuwa akizungumzia alivyohisi kama Pablo alipokuwa akishughulikia viatu vyake, alijihisi kama alivyohisi Pablo alipokuwa akiangaziwa kwenye habari,” ameambia BBC.

“Nilifikiria kwamba alikuwa anazungumzia Pablo Escobar au Pablo Picasso.

“Kwa hivyo nikafikiria lazima iwe The Life of Pablo.”

Dante anatoka New Jersey nchini Marekani na ni mwanarepa na produsa wa muziki. Anafanya kazi na HW4L Records.

Alifrahi sana alipogundua kwamba alikuwa amepata swali hilo kuhusu TLOP.

Kanye West

“Simu yangu ilianza kuita. Nilifikiria Kanye alikuwa ametangaza jina kamili na lilikuwa The Life of Pablo,” anakumbuka.

“Watu walinipigia kila mmoja akiniambia, ‘Umeshinda, umeshinda’. Nilifurahi sana. Singetarajia hilo.”

Dante anasema wahudumu wa Kanye hawajawasiliana naye bado.

Lakini atatumia zawadi hiyo kusaidia watu wasiojiweza.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s