DMX atoka hospitalini baada ya kuokolewa

Nyota wa muziki wa Hip Hop nchini Marekani DMX ametoka hospitalini baada ya kushindwa kupumua na kulazimika kusaidiwa kufanya hivyo katika eneo la kuegesha magari ndani ya hoteli moja mjini New York.

 dmx

Wakili wa nyota huyo wa Rap, Murray Richman amethibitisha kwamba amepona baada ya kuanguka katika mji wa Yonkers siku ya jumatatu.

Bwana Murray amesema kuwa hakujua kilichosababisha msanii huyo kushindwa kupumua lakini akaongezea kwamba anaugua pumu.

Msemaji wa polisi wa eneo la Yonkers aliiambia Newsbeat kwamba maafisa walimpata mtu mwenye umri wa miaka 45 ndani ya gari.

Wafanyikazi wa Ambiulensi walimpatia dawa inayoitwa Narcan ili kumuokoa na baadaye alipelekwa hospitalini mda mchache baadaye.

Satish Palav,meneja wa usiku wa mgahawa wa Ramada inn huko Yonkers alithiibitishia Newsbeat kuwa DMX alikuwa akiishi hapo.

”Baadaye ambiulensi iliwasili na kuja kumchukua”.

 Hoteli ya Ramada

Alisema kuwa mwanamuziki huyo aliingia katika hoteli hiyo tarehe mosi mwezi Februari lakini hajarudi tangu alipopelekwa hospitalini.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s