NMB na Care International wazindua Pamoja Account

Benki ya NMB imezindua rasmi bidhaa ya Pamoja Account kwa kushirikiana na CARE International kusaidia vikundi vya kijamii vyenye lengo moja kwa maendeleo ya pamoja.

12717651_838807826229654_3311873107246046210_n

Akizungumza na waandishi wa habari katika zoezi hilo Oliva kinabo mkurugenzi wa Jinsia na maendeleo ya wanawake kutoka katika shirika la Care international amesema kuwa shirika lao walipewa mapendekezo na vikundi vingi ambavyo wanafanya navyo kazi kwa wanakikundi kuwa wanahitaji kutunza pesa zao kisasa ndipo walipoonelea kuwatafuta NMB na kufungua akaunti hiyo.

11933450_838807679563002_3648765540480725172_n

Naye Bi Joseline Kamuhanda kutoka NMB alieleza kuwa walipokea wazo hilo kwa mikono miwili na kuamua kulifanyia kazi kwa kuwa wao jukumu lao ni kuwahudumia wateja wake, kwahiyo haikuwaa ngumu kuanza kufungua akaunti hiyo ya Pamoja ambayo inawawezesha wanavikundi kuweka pesa zao katika akaunti moja.

Aidha ailongeza kuwa wao kama NMB wataendelea kutoa huduma ya NMB CHAP CHAP kwa kila mwanakikundi na itawawezesha wanakikundi kuweza kuweka pesa zao kwa njia ya simu popote pale walipo.

Kwa upande wa baadhi ya wanavikundi ambao wako chini ya Care International wamepongeza hatua hiyo na kusema Care na NMB imewasaidia katika kuweka pesa zao zikiwa salama kwa kuwa awali kulikuwa na matukio kadha wa kadha ikiwa kama kuibiwa na wezi, wanavikundi wenzao ma hata wazazi wenzao huko majumbani mwao.

12743848_838807786229658_9183152237288508674_n
Baadhi ya viongozi wa vikundi vya kuweka na kukopa ambavyo viko chini ya Care international ambavyo vimejiunga na Pamoja Accaunt.

Shirika la care international lilinanza kazi hapa nchini mwaka 1994 hadi leo na linafanya kazi Zaidi ya nchi 90 likiwa na lengo la kuinua jamii kiuchumi ndipo lilipoonelea kuanzisha vikundi vya kuweka na kukopa, hadi sasa limeweza kutengeneza vikundi elfu 20 vikiwa na wanachama laki nne nchi nzima.

 

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s