Wakuzaji bangi wakutana Israeli

Wataalamu wanaohusika na matumizi ya bangi kama dawa wanakutana Israel kujadili uvumbuzi zaidi katika kilichokuwa sekta yenye thamani ya mabilioni ya dola duniani.

 160302182501_cannabis_general_main_624x351_epa_nocredit

Hayo ndiyo maazimio ya Canna-Tech inayojumuisha wawekezaji, wakulima halali na watumizi wa bangi kama dawa.

Uwekezaji katika sekta hiyo umekuwa kwa kasi ya juu mno kufuatia uhalalishwa kwa bangi katika majimbo kadhaa nchini Marekani.

Nchini Israeli sekta hiyo ya bangi halali imefunguka na inaelekea kukua kufuatia utafiti na uwekezaji mkubwa.

Afisa mmoja anayesimamia utafiti huo Saul Kaye anasema

”Wagonjwa ni watu wanaopata matibabu ya maradhi ambayo yanapatikana baada ya kutumia kemikali yenye madhara kama vile ugonjwa wa Saratani.


Watu hao ni wale wanaougua ugonjwa wa kusahau, ugonjwa wa Crohn, na wale walio na msongo wa mawazo au mfadhaiko.

Bangi inaweza kusaidia matatizo kama hayo, na bado hatujajua manufaa mengine.

Utafiti unahitajika zaidi, jambo ambalo Israeli inaendelea kuchunguza hasa katika ngazi ya shirikisho

Kwa sasa, kuna utafiti zaidi ya 36 unaoendelea katika hospitali nchini Israeli. ”

Biashara hii ya bangi iliyoanzishwa kwa njia ya soko la magendo, na wafanyibiashara wa awali walitokea hapo.

Lakini kuna kampuni mahususi ya uundaji madawa, katika soko la hisa la Wall Street Marekani sasa yanaangazia biashara ya bangi, hapo ndipo tunaivalia njuga, na bila shaka tunaanza kubadili mtizamo kuhusiana na biashara ya bangi.” alisema Kaye.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s