Kuchati ni marufuku katika wizara TZ

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini Tanzania imewapiga marufuku wafanyakazi wake ”Kuchati” katika mitandao ya kijamii kwa kutumia simu katika muda wa saa za kazi.

 141126171416_whatsapp_blogger_624x351_bbc

Waziri wa Wizara hiyo Makame Mbarawa amekemea tabia ya baadhi ya wafanyakazi, kutumia muda mwingi maofisini kuperuzi katika mitandao ya kijamii pamoja na kupiga porojo, hali inayosababisha kushuka kwa uzalishaji na maendeleo.

Ameongeza kuwa watakaobainika kufanya hivyo watachukuliwa hatua za kisheria bila ya kuonewa haya, na pia kuwataka wafanyakazi wa wizara yake kuwa na bidii ya kazi na weledi

Lakini hata hivyo, marufuku hiyo itaweza kufanikiwa?, kutokana na ukubwa wa matumizi ya mtandao, huku walengwa wakiona wananufaika nayo.

Kutokana na kukua kwa teknolojia ya habari na mawasiliano duniani, watu wengi hususan vijana wamekuwa wakitumia muda mwingi katika mitandao ya kijamii, kupitia simu za mikononi na kompyuta, kwa lengo la kupata taarifa mbalimbali za ulimwengu na pia kujifunza.

Nchini Tanzania matumizi ya huduma ya mawasiliano imekuwa kwa kasi katika siku za hivi karibuni, hususan kupitia mitandao ya WhatsApp, Facebook, Twitter na blogi mbalimbali.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s