Shirika la Young Strong Mothers Foundation lasaidia waliopata mimba mapema Tanzania

Mimba za utotoni ni tatizo kubwa katika nchi nyingi zinazoendelea, zikiwepo nchi za Afrika Mashariki.

 160308180404_young_strong_mothers_foundation_founder_640x360_bbc

Young Strong Mothers Foundation ni asasi inayosaidia wasichana zaidi ya 200 walioshindwa kuendelea na masomo mjini morogoro, Mashariki mwa Tanzania.

Leo ikiwa siku ya wanawake duniani, mimba za utotoni ni miongoni mwa changamoto ambazo zinawarudisha nyuma wanawake katika harakati zao za kuleta maendeleo.

Mabinti wadogo wanakatizia njiani masomo yao kwa kuwa wanapata mimba wakiwa na umri mdogo na kupelekea kufukuzwa shule, kufukuzwa na wazazi na jamii kuwanyooshea kidole.

Hukumu kubwa ambazo wanazipata kutoka katika jamii inayowazunguka inawezekana huwalenga wao kimakosa kwa kuwa sio wao pekee wakulaumiwa kwa sababu wana nyingi zilizowafanya kutumbukia kwenye adha hiyo.

Helmina Msaliwa ana umri wa miaka miaka 20 na mtoto wake ana miaka mitatu, anasema alimpata mtoto wake bila matarajio kutokana na hali ngumu ya maisha, mazingira yaliyosababisha akapata ujauzito na kufukuzwa nyumbani pamoja na shule

Hata hivyo mbaya zaidi kuhusiana na mimba za utotoni ni kwamba wengine hujikuta katika hali hiyo kutokana na kubakwa.

Amina Juma mwenye umri wa miaka 21 ambaye ana mtoto wa miaka minne, aliyelelewa na bibi yake hivyo ilimlazimu kufanya kazi za ndani ili aweze kujilipia karo ya shule lakini matokeo yake aliishia kubakwa na kusitisha masomo yake.

Ugumu wa maisha kwa ujumla mwishowe unadaiwa kuwaingiza baadhi ya wasichana katika biashara ya kujiuza ili waweze kukidhi mahitaji yao na kuwalea watoto wao.

Zamoyo Seif amejikuta katika ukurasa huo. Baada ya wazazi wake kutengana na hali kuwa mbaya zaidi pale ambapo mzazi mmoja alipobaki na jukumu la kumlea, aliamua kutoroka na mwishowe akaingilia biashara ya kujiuza.

Jackie Bomboma ni mkurugenzi kutoka asasi ya Strong Mothers Foundation, na ambaye amesema amepitia historia inayofanana kwa sehemu fulani na mapito ya wasichana waliotumbukia katika mimba za utotoni.

Yeye ana umri wa miaka 29 na mtoto wake mwenye umri wa miaka 14.

Jackie anasema hali ngumu ambayo aliyoipitia tangu wazazi wake walipofariki na kukosa usaidizi kutoka kwa jamii yake ndio ilimpelekea kupata mimba akiwa na umri mdogo.

Hali hiyo ngumu aliyoipitia ilimfanya asukumwe kuwasaidia mabinti hao kwa kuwa anaamini kuna sababu nyingi zilizowapelekea kuingia kwenye janga hilo.

Shirika hilo la Young Strong Mothers Foundation bado linakumbana na changamoto ya kupata ufadhili wa kuweza kuwakwamua wamama hao wadogo pamoja na watoto wao kuondokana na hali ya unyanyapaa wanayokutana nayo kutoka katika jamii.

Hali kadhalika shirika hilo linaiomba serikali kuweza kurekebisha sera yake ya elimu ili wasichana wenye umri mdogo wanaopata mimba waweze kuendelea na masomo.

Kwa sasa shirika hilo limeweza kuwapeleka wamama wadogo 15 katika shule ya ufundi wa fani mbalimbali kama ufundi cherehani, mapishi, umeme na nyinginezo huku wengine wakiwa wanapata ushauri wa ujasiriamali na masuala ya afya.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s