Magufuli apiga simu kituo cha runinga”Clouds TV”

Rais wa Tanzania John Magufuli amewashangaza wengi baada ya kupiga simu katika kituo cha runinga asubuhi.

 160317115223_magufuli_waves_640x360_bbc

Rais huyo alipiga simu wakati wa kipindi cha Clouds 360 kueleza kufurahishwa kwake na kipindi hicho.

Tangu kuingia madarakani Novemba mwaka jana, kiongozi huyo hajafanya mahojiano yoyote ya moja kwa moja na kituo chochote cha habari.

“Mimi nawapongeza sana kwa kweli,” alisema Dkt Magufuli, kabla ya kuendelea na kutaja majina ya watangazaji wa kipindi hicho na kusema huwa wanachambua vyema magazeti.

Alisema aliwapigia simu kuwapongeza.

Mmoja wa watangazaji hao alichukua fursa hiyo kumuuliza swali Dkt Magufuli.

Swali lilihusu kutolewa kwa zawadi kwa wanawake lakini Dkt Magufuli alishangaa ni kwa nini hawakuwapa wanaume zawadi.

Baada ya kumaliza kuzungumza, Dkt Magufuli alimkabidhi simu mkewe Janet ambaye pia alieleza furaha yake kuhusu kipindi hicho.

“Yaani mnatupa faraja, huwa tunacheka sana na mzee wangu hapa,” alisema Bi Magufuli.

Baadaye alirejesha simu kwa Dkt Magufuli ambaye kwa utani aliwashauri watangazaji wakati mwingine wajitokeze na wachumba wao.

“Sam (Sasali) na mke wake, Babbie (Kabae) aje na mume wake na wewe Hudson (Kamoga) uje na mke wako hapo. Siku nyingine mwakaribishe hapo,” alisema.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s