Kupanda na kushuka kwa simu za Nokia

Je, unaikumbuka siku za Nokia na enzi zake? Sasa Jina Nokia linatokaka na mji mdogo nchini Finland, ambapo simu hiyo iliyokuwa maarufu duniani iligunduliwa.

 160318142506_nokiagofigure3

Kuna dalili kidogo kuwa mji huo mtulivu wakati mmoja uliipa simu jina lake, simu ambayo ilibadili kabisa sekta ya simu mapema miaka ya tisini na kubadilisha kabisa uchumi wa Finland kuufanya kuwa uchumi ulioboreka kwa haraka zaidi duniani.

Wakati ikiwa katika kilele chake kwa mapema miaka ya 2000, Nokia iliuza asilimia 40 ya simu zote duniani ambapo ilitambuliwa na kuwa simu maarufu zaidi duniani.

Nchini Finland kwenyewe matokeo yalikuwa hata makubwa. Kulingana na taasisi inayofuatilia uchumi wa Finland ni kuwa simu za Nokia zilichangia robo ya uchumi wa nchi hiyo kati ya mwaka 1998 na 2007.

Lakini kwa ghafla soko la simu za Nokia lilishuka kwa kishindo na mauzo kudorora kabisa hali hiyo iyoathiri pakubwa uchumi wa Finland na pia kusabibisha kuwepo kipindi kigumu na kirefu kwa uchumi wa nchi hiyo.

“Nokia ilikuwa ni uti wa mgongo wa kila kitu hapa , kuanguka kwake ilikuwa ni kama jinamizi kwa taifa la Finland kwa mujibu wa mkurugenzi wa uchumi na maendeleo ya mji wa Tampere, Kari Kankaala, mji ulio umbali kidogo kutoka Nokia.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s