Hiki ndio kiatu ambacho raia wa misri kinawakera

Hatua ya mchezaji maarufu wa soka duniani Lionel Messi kutoa viatu vyake viuzwe kusaidia watu wasiojiweza imeibua mjadala mkali nchini Misri.

 160330100813_messi_mtangazaji_512x288_bbc_nocredit

Messi alifanya hivyo akidhani labda kwamba alikuwa anafanya hisani bila kufahamu kwamba viatu huwa na maana nyingine nchini Misri na pia katika mataifa ya mengine ya Uarabuni.

Wakati wa mahojiano ya runingani ”katika kipindi cha Yes am Famous” kinachopeperushwa hewani na runinga ya MBC Misri, mchezaji huyo wa Argentina aliwaambia watangazaji hao kwamba angependa kutoa viatu vyake vipigwe mnada.

Kitendo chake kilipokelewa tofauti kabisa na wiki chache zilizopita alipopongezwa na kusifiwa sana kwa kutimiza ndoto ya kijana mmoja wa Afghanistan alipomtumia mpira na fulana yake.

 

Alipokuwa akivitoa viatu vyake Misri, hakujua kwamba viatu huchukuliwa kama matusi au kukosea watu heshima katika maeneo mengi ya Mashariki ya Kati.

Muda mfupi baadaye wakazi wa maeneo hayo walimkashutumu sana kupitia mitandao ya kijamii.

Na ili kujibu matusi hayo mbunge mmoja wa Misri said Hassin anayetangaza kipindi kwa jina ‘Infirad’ alitoa kiatu chake na kusema kwamba atampatia Messi.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s