Mzaha wa Google Siku ya Wajinga waleta balaa

Google imelazimika kuondoa kitufe cha Siku ya Wajinga kutoka kwenye huduma yake ya barua pepe ya Gmail baada ya watu wengi kulalamika.

 160401122102_google_april_fool_button_624x351_getty

Kitufe hicho kilikuwa kinatuma video za mzaha kwa watu walio kwenye anwani ya mtu.

Kitufe hicho kilikuwa kimewekwa karibu na kitufe cha kawaida cha kutuma barua pepe na kiliwawezesha watumizi wa Gmail kusitisha mawasiliano ya kawaida na badala yake kutuma video fupi ya gif ya kibonzo kikiweka chini maikrofoni.

Image copyright Gmail

Watu wengi wamelalamika sana kuhusu kitufe hicho kwenye kumbi za Google.

Kuna wanaosema wamefutwa kazi baada ya kuwatumia wakubwa wao barua pepe za mzaha, wengine wanasema wametuma barua pepe za mzaha kwa kampuni ambazo walikuwa wanaomba kazi.

Mwandishi mmoja aliandika kwamba alikuwa anataka kutuma makala zake kwa mhariri na muda ulikuwa unapita akatuma haraka. Alisubiri jibu lakini hakupata. Baadaye aligundua kwamba kimakosa alibofya kitufe cha mzaha.

Kampuni hiyo imeondoa kitufe hicho na kuomba radhi.

“Inaonekana kana kwamba tumejitania sisi wenyewe mwaka huu,” Google imesema kupitia taarifa.

“Kutokana na hitilafu katika utengenezaji wa kitufe hiki, kiungo cha kuweka maikrofoni chini (MicDrop) kilisababisha kilio kuliko kicheko. Tunaomba radhi.”

Google ilitangaza kuanzishwa kwa Gmail tarehe 1 Aprili 2004 na wakati huo wengi walidhani ulikuwa mzaha wa Siku ya Wajinga.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s