Magari nane yavunjwa ufanyaji video ya Sugu

Mbunge wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya CHADEMA Joseph Mbilinyi A.K.A Sugu amethibitisha kuvunjwa kwa magari nane na vibaka wakati wa ufanyaji wa video ya wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ‘Freedom’

Sugu%20

Jana kupitia ukurasa wa Facebook wa msanii G Solo alisema kuwa wanashukuru Mungu kwa kukamilika kwa video ya wimbo mpya wa Sugu na kusema kuwa wamesikitishwa na kitendo cha vibaka kuvunja magari yao na kuiba vitu mbalimbali kama Laptop, simu, Ipad, mabegi ya nguo, pesa.

“Freedom video iliisha salama tuna mshukuru mungu ila, tukio la wizi lililotokea limetusikitisha wengi na ni ushenzi wa hali ya juu! magari nane kuvunjwa vioo na kuibwa vitu mbalimbali zikiwemo simu, laptops, ipad, mabegi ya nguo, pesa nakadhalika. siwezi kusema ni vijana wa Ununio ila yeyote aliye husika na alaaaniwe”. Aliandika G Solo.

G%20Solo%20

Leo Mbunge huyo wa Mbeya Mjini amethibitisha kutokea kwa wizi huo na kusema kuwa wanakomaa nao waliofanya tukio hilo na kudai kuwa kama wangejua kuwa magari hayo yalikuwa ya masela zaidi yao wasingethubutu kufanya jambo hilo.

” Mzigo utakuwa wa maana kwani shooting ilikuwa poa sana. Isipokuwa kwa vibaka waliozingua kwa kuvunja magari mwishoni. Asante sana na tunakomaa nao. Wangejua waliokuwemo ndani ni ‘Masela’ zaidi yao wasingethubutu” alisema Joseph Mbilinyi.

Video mpya wa Sugu ambayo bado haijafahamika itatoka lini imeongozwa na Director Hanscana.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s