Mpende akupendaye asiyekupenda achana nae- Jokate

Mwanzoni mwa mwaka kulikuwa na tetesi kuwa Jokate Mwegelo na Ali Kiba walikuwa wanatoka kimapenzi lakini siku zinavyozidi kwenda kumekuwa na utata juu ya watu hao kama bado wapo pamoja au kila mtu amechukua hamsini zake.

Jokate%20

Jana kupitia kipindi cha eNEWS Ali Kiba aliulizwa kama anatoka kimapenzi na Jokate na majibu yake yalizidi kuleta utata kwani alisema kuwa siku zote amekuwa akizungumza kwenye vyombo vya habari kuwa yeye na Jokate Mwegelo ni marafiki na si wapenzi.

Lakini akasema “Vijana siku hizi tumekuwa tukisahau njia walizotumia wazazi wetu kuwapata wake” na kusema wao walianzia kuwa marafiki kwanza kabla ya kuoana kwani ni rahisi sana kwa wapenzi kuachana lakini ni vigumu kwa marafiki kuachana au kutengana.

Jojo%20

Leo Jokate Mwegelo ameanza kwa kupost ujumbe ukisomeka kama Mpende akupendae na asiyekupenda achana naye na baadaye akaweka ujumbe ukitoka kwenye wimbo wa Lady Jaydee wa ‘Ndi Ndi Ndi’ akisema: “Niliwezaje kutoa vyote ili hali wewe ulininyima vyote, kama ni jipu lilivimba zaidi”

“Niliwezaje kutoa vyote ili hali wewe ulininyima vyote, kama ni jipu lilivimba zaidi. Nikasahau chizi huwa haponi kama chozi mvuani. Hatimaye kumekucha na milembe nimekushusha. Na geti likifungwa naondoka” Aliandika Jokate.

Kitendo hiki kimeibua hisia kwa mashabiki na kudhani kuwa huenda wasanii hawa hawapo sawa kwa sasa huku wengine wakihisi kuwa ujumbe huo labda amewekewa King Ali Kiba.

“Jojo unatakiwa uwe na mtu wa kujielewa achana na wasanii kabisa, tulia atakuja wa kufanana na wewe si umeona wakina Faraja Nyarandu Please Please Jokate Mwegelo” alisema shabiki wake Dorry Quhey.

“Tayari umeshawekwa kapuni, shida zetu mnapenda . Mimi nilikupenda hata kabla hujawa Miss Tanzania” Mkambaku_jr

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s