Meya Kinondoni: Utumbuaji majipu hauepukiki.

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mh. Boniface Jacob mapema leo Mei 5.2016 ametangaza kuwasimamisha kazi watumishi wawili wa Manispaa ya Kinondoni, akiwemo Mwanasheria Mkuu BW. Burton Mahenge na Mthamini wa Manispaa Bw. Einhard Chidaga baada ya Madiwani kuamua kwa kauli moja kuwachukulia hatua hiyo.

Meya-Jacob

Akisoma taarifa na nyaraka mbalimbali mbele ya wanahabari, Mh. Boniface Jacob alieleza kuwa: Kikao cha Kamati ya fedha na Uongozi cha tarehe 29/04/2016, kiliagiza kuwa yaorodheshwe mashauri yote ambayo hayakusimamiwa vizuri na Mwanasheria wa Manispaa Bwana Burton Mahenge, na hivyo kuisababishia Manispaa kupata hasara, kupoteza mali, na kuchelewa kupata manufaa katika mali zake.

Mashauri hayo aliyaorodhesha kuwa ni pamoja na kushindwa kukata rufaa kwa shauri la fukwe ya coco beach, na kutokea kasoro kadhaa katika baadhi ya mikataba ya almashauri hiyo, na kuongeza kuwa atasimamishwa kupisha uchunguzi na mahojiano ambayo yatafanywa dhidi yakechini ya vyombo vyote vya kisheria, huku hakiwataka wanasheria ambao wanamapenzi na kinondoni kujitokeza kuisaidia almashauri hiyo katika msaada wa kisheria.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s