Global Peace Foundation Tanzania: Vijana Na Amani

Shirika la Global Peace Foundation Tanzania limewataka vijana wa kitananzania kutumia vizuri mitandao ya kijamii katika kudumisha na kulinda amani ya taifa, ambayo ni tunu kubwa ya taifa la tanzania na endapo itatoweka ni kazi kubwa kuirejesha.

DSCN0272

Country Director Martha Nghambi

Hayo yalizungumzwa na mkurugenzi mkazi wa Global peace Foundation Tanzania Martha Nghambi wakati wa warsha ambao iliandaliwa katika chuo kikuu cha Dar es salaam katika kitivo cha habari, ambapo dhumuni kuu lilikuwa ni jukumu la vyombo vya habari katika kulinda na kudumisha amani Tanzania.

Taasisi hiyo ilizungumza kwa njia ya mdahalo na wanafunzi katika chuo kikuu dar es salaam ambao wanasoma masomo ya waandishi wa habari na kuweza kuibua changamoto nyingi na nini kifanyike ili vijana waweze kupambana na masuala ya uvunjifu wa Amani katika tasnia ya habari.

DSCN0347
Munira Hussein mwanafunzi chuo kikuu Dar es Salaam kitivo uandishi wa habari.

Mmoja kati ya wanafunzi hao munira Hussein alisema kuwa waandishi wa habari wana nafasi kubwa katika kulinda Amani, huku akitolea mfano mauji ya kimbali ambayo yalifanyika nchini Rwanda mwaka 1994 kuwa yalichangiwa na vyombo vya habari. “Sisi waandishi tunaweza kuifanya jamii ya watu kuwa na maono mazuri kama tutatumia kalamu zetu vizuri”.

DSCN0330
Anthony Luvanda mmoja ya wanaharakati vijana alikuwepo katika warsha hiyo.

Kwa upande wake moja ya wageni rasmi alikuwapo Anthony Luvanda ambaye ni mwanaharakati na amewataka vijana wa kitanzania ambao wako katika tasnia ya habari kuifanya kisasa kwa kuweka vitu chanya na kuongeza kuwa mtu ambaye anataka kusomea uandishi wa habari basi awe na moyo na msukumo wa kuisomea kwani mwandishi wa hjabari mwenye wito wake atafanya kwa moyo wake woto, na watu makini ufuta maono yao.

Shirika la Global peace foundation limekuwa likijitokeza mara kwa mara katika kupigania Amani kwa watanzania, kwa kuandaa warsha mikutano mbalimbali katika kuhakikisha nchi inakuwa ya Amani na utulivu.

DSCN0259DSCN0296DSCN0354DSCN0396DSCN0364DSCN0362DSCN0338DSCN0337DSCN0336DSCN0326DSCN0293

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s