Zitto Kabwe aitaka serikali kuhakikisha vituo vya Redio na Tv vinacheza nyimbo za wasanii wa nyumbani kwa 80%.

Baada ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia Waziri mwenye dhamana Nape Nnauye kuwasilisha Bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2016-2017 ambapo wizara hiyo iliomba kuidhinishwa kwa kiasi cha  shilingi 20,326,176,000 kwa mwaka wa fedha 2016-2017,Wabunge mbalimbali wamekua wakichangia bajeti hiyo ambapo mbali na wabunge wengi kukosoa utendaji wa wizara hiyo juu ya ile issue ya uhuru wa habari hasa katika kipindi hiki ambacho mikutano ya bunge imesitishwa kuoneshwa live,kwa upande wake Mbunge wa Kigoma mjini kwa tiketi ya chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe aliibua hoja mpya wakati wa uchangiaji kwa kumtaka Waziri wa wizara husika kuhakikisha vituo vya redio na Tv nchini kuhakikisha wanacheza nyimbo za wanamuziki wa ndani.

zito bungeni 001                                                       Zito Kabwe.

“Leo hii ukifungua Redio au TV za hapa nyumbani zote asilimia nyingi utakuta wanapiga nyimbo za nje tu. Leo hii ukienda nchi za watu kuna limit mfano ukienda Lagos,Nigeria ukisikia nyimbo ya msanii wa huku kwetu basi ujue lazima atakuwa amefanya na msanii wao yaani wana promote wasanii wao, sasa sisi sijui ni ulimbukeni wa ukoloni wa miaka hamsini bado haujatutoka. Nape hili lipo kwako kama unataka kuwatetea wasanii hili wala halihiitaji kubadilisha sheria na kanuni za kontenti zipo chini ya waziri. Toa kanuni TCRA wazibariki kuwa asilimia 80 ya nyimbo zitakazopigwa kwenye redio na TV zetu ziwe za wasanii wetu wa Tanzania basi,” alisema Zitto ambae pia ni kiongozi mkuu wa chama cha ACT.

zito na baba levo 001   Zitto Kabwe(R) na Baba Level  mmoja wa Madiwani wa chama cha A.C.T ambaye pia ni Mwanamuziki.

zito na Linex 002                                                Zitto Kabwe(L) na Linex.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s