Rasilimali watu na Fedha ni Changamoto kubwa TAZARA: Betram KIswaga

SHIRIKA la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA) linakabiliwa na Changamoto za Rasilimali watu pamoja na mitaji ya fedha ambapo changamoto hizo zimepelekea shirika hilo kutofikia malengo yake.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Kaimu mkurugenzi mkuu wa (TAZARA) Dkt Betram Kiswaga wakati wa uzinduzi wa kitabu kinachozungumzia histori ya shirika hilo tangu lianza kufanya kazi kwenye miaka ya 1970 ambapo kitabu hicho kimeandaliwa na nchi ya China ambao ndio waliotengeneza reli kutoka Tanzania hadi Zambia.

Tazara+clip

Dkt Kiswaga amesema TAZARA linashindwa kwenda na kasi ya ufanyaji kazi ambao ungeweza kuliingizia taifa mapato.

Kiswaga amefafanua kuwa kutokuwepo na rasilimali watu wenye sifa na utaalamu kumechangia shirika hilo kushindwa kujiendesha vizuri.

“Nina mwaka mmoja kwenye Tazara ila shirika hili limeshiindwa kufanya kazi kama tunavyotaka kutokana kutokuwa na wataaalumu wenye sifa huku wengi wakiacha kufanya kazi na Tazara kutokana na shirika kutokuwa na mitaji ya fedha ambayo ingeweza kuwamudu wataalamu”amesema Dk Kiswaga.

Hata hivyo,Dk Kiswaga amesema licha ya kukumbuna na changamoto hizo,amedai bado shirika hilo linaendelea na kutoa huduma ya usafiri kutoka Tanzania na Zambia huku akitoa Pongezi kwa nchi ya China kuendelea kutoa ushirikiana kwa shirika hilo.

Naye Balozi wa China nchini LU Youqing amesema Serikali ya China itaendelea kutoa ushirikiana kwa shirika hilo.

Amesema kwa sasa wanafahamu shirika hilo linakumbana na changamoto jambo analodai kuwa nchi yake hatosita kulisaidia shirika hilo katika kuzitatua changamoto hizo.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s