JKCI na BLK yafanya upasuaji mkubwa wa moyo kuwahi kutokea Afrika mashariki na kati.

Taasisi ya moyo ya jakaya kikwete kwa kushirikiana na hoaspitali ya BLK kutoka nchini india kwa mara ya kwanza imefanya upasuaji mkubwa wa moyo kwa kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (bypass surgery) bila ya kuusimamishaa moyo kwa akutumia amashine maalum inayoitwa heart lung machine.

001

 

Akizungumza na waandishi wa habari mkurugenzi kaimu mkurugenzi wa taasisi hiyo dr. Peter Kisenge amesema kuwa upasuaji huo ni wa kwanza kufanyika nchini Tanzania, Africa mashariki hata na kati pia, na kuongeza kuwa wataalamu hao ni kwa mara ya tatu sasa wamefanikiwa kutoa tiba kubwa bila moyo kupasuliwa kwa kutumia mtambo wa cathlab kwa kuzibua valvu zilizoziba (BMV procedure).

003

Wataalamu hao watakaa kwa siku mbili Zaidi na kutoa mafunzo kwa watoa huduma pamoja na kumalizia upasuaji kwa wagonjwa wengie ambapo watakamilisha hesabu ya watu na kufikia 18 na kuweza kuokoa takribani Zaidi ya shilingi millioni 180 kama wagonjwa hao wangepelekwa nje ya nchi kwa matibabu kama hayo.

004

Mbali na kutoa taarifa hiyo pia taasisi hiyo imesaini hati maalum ya ushirikiano na taasisi ya BLK ya nchini india kwa ajili ya kuwapa mafunzo watumishi wake na kuendelea kutoa huduma ya uapsuaji huo wa moyo.

Aidha taasisi hiyo kwa mwaka huu imeweza kufanya procedure 471 ikiwemo upasuaji wa moyo kwa kufungua kifua (99), vipandikizi (78), vizibua njia (265), na nyinginezo (29).

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s