Global Peace Foundation Tanzani yalaani mauaji yanayoendelea nchini.

Taasisi isiyo ya kiserikali Global Peace Foundation Tanzania kwa kushirikiana na wadau wa Amani nchini wanalaani vikali na kupinga vitendo vyovyote vya uvunjifu wa Amani nchini vinavyopelekea uhalifu dhidi ya maisha ya binadamu na ustawi wa maisha yao.

Global-Peace-Foundation-Logo2

Akizungumza na wanahabari mkurugenzi mkazi wa global peace foundation tanzani Martha nghambi amesema kuwa hivi karibuni kumeripotiwa na vyombo vya habari kuwepo kwa matukio kadhaa ya mauaji ya binadamu likiwamo tukio la mauaji ya wanafamilia saba na tukio la shinyanga la mauaji ya watu watatu katika msikiti wa Rahman mkoani mwanza.

“Tukio la alhamis tarehe 19/05/2016 ambapo watu wasiojulikana walivamia msikiti wa Masjid Rahman nan a kuua watu watatu huku wakijeruhi watu wengine na wauaji kutokomea kusikojulikana pamoja na tukio lililotokea wilaya ya sengerema mkoani mwanza ambapo wanafamilia saba walivamiwa na kuuwawa kwa kukatwa na mapanga na pia wauaji kutokomea kusikojulikana pia tunalaani vikali”, alisema Martha Nghambi.

Aidha aliongeza kuwa tukio jingine ambalo lililotokea mnamo tarehe 19 mwezi huu nje kidogo ya jiji la dar es salaam maeneo ya mwandiga kulitokea na mauaji ya jeshi la polisi aliyekuwa nyumbani kwake sajent Ally Kinyogori ambaye alipigwa risasi na watu wasiojulikana, “Imefika hatua sasa wapenda Amani wote sasa nchini kuungana kwa ujumla kulaani na kupinga vitendo hivyo vya kinyama vilivyopelekea kupoteza maisha kwa raia wenzetu”, Alisema Martha.

Taasisi hiyo imelipongeza jeshi la polisi kwa juhudi zake za kupambana na wahalifu hao, huku likiwataka watanzania kuwa mabalozi wa Amani na kuwafichua wahalifu na kuitaka serikali na vyombo vya usalama kuona washtakiwa wote wanafikishwa kwenye vyombo vya sheria na sheria ichukue mkondo wake.

Global Peace Foundation Tanzania ni taasisi ambayo imekuwa ikishiriki mara kwa mara katika kulinda, na kuitunza Amani mara kwa mara kwa kuandaa warsha, mikutano na makongamano jamii, huku mara ya mwisho iliandaa warsha katika chuo kikuu cha Dar es salaam katika kitivo cha habari, ambapo dhumuni kuu lilikuwa ni jukumu la vyombo vya habari katika kulinda na kudumisha amani Tanzania, huku kauli mbiu ikiwa vijana na amani.

 

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s