Water Aid Foundation Kuendelea kusaidia shule duni.

Shirika lisilo la kiserikali Water Aid Foundation limesema litaendelea kutoa misaada katika shule za msingi na sekondari ambazo zenye miundombinu mibovu ya maji, vyoo na Afya kwa ujumla ili kumhakikishia mtoto elimu bora ambayo itaambatana na Afya.

20160527_115242

Hayo yamesemwa na meneja mradi  leo Clare Haule katika shule ya msingi Mchangani iliyoko mwananyamala wilaya ya kinondoni jijini Dar es salaam wakati wa sherehe ya maandalizi ya kuelekea siku ya edhi salama ambayo kilele chake siku ya kesho tarehe 28 ambapo walikuwa wanakabidhi choo katika shule hiyo na msaada wa pedi kwa watoto wa kike.

Aidha amesema kuwa katika shule nyingi nchini Tanzania kumekuwa na hali mbaya katika shule nyingi kiafya na mazingira rafiki kwa waatoto wa kike hali ambayo hupelekea wanafunzi wengi wa kike kutoudhuria masomo pindi wanapokuwa katika siku zao za edhi.

20160527_110836

Naye mratibu huduma ya maji, elimu, na usafi wa mazingira mashuleni Theresia Kiwike kutoka wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia amesema kuwa awali kabla ya kuanza kutoa misaada mashuleni kulikuwa na hali mbaya sana “Watoto walikuwa hawaendi mashulenikatika siku zao za edhi ila baada ya kuanza kutolewa misaada ya pedi na kujengwa kwa vyoo ambavyo ni rafiki kwa watoto wa kike na shirika la water aid maudhurio ni mazuri”, Alisema bi. Theresia.

Siku ya edhi salama hufanyika kila tarehe 28 ya mwezi wa 5 kila mwaka ambapo kesho itafanyika kitaifa jijini Dar es salaam huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam mh. Paul makonda, huku kukitanguliwa na maandamano ya amani yatakayo anzia wizara ya elimu sayansi na Teknolojia ya kiishia katika viwanja vya mnazi mmoja.

 

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s