Gloabal peace Foundation Tanzania yafundisha watoto kuishi kwa amani

Shirika ambalo si la kiserikali Global Peace Foundation Tanzania lenye makao yake nchini marekani na lenye matawi zaidi ya 20 duniani leo lilitembelea katikaShule ya awali Crystal Wonderland iliyopo Sinza Dar es salaam katika muendelezo wa kampeni ya ‘vijana na amani’ na kutoa elimu kwa watoto jinsi ya Kuishi vema ili kuilinda na kuidumisha ‪‎amani ya Tanzania.

IMG-20160530-WA0001

Katika ziara hiyo mkurugenzi mkazi wa Global Peace foundation Martha Nghambi amesema kuwa wameamua siku ya leo kutembele shule hiyo kwa kuwa utoto ni mwanzo wa Ujana, kumjengea Mtoto Utamaduni wa kupenda amani ni kumuandaa kuwa Balozi wa amani pindi atakapo kuwa mkubwa ni jambo la muhimu sana. Aliendelea pia na kutoa mfano wa msemo maarufu usemao “Samaki mkunje angali mbichi”.

Alisema kuwa lengo kuu siku ya leo lilikuwa ni kuwajenga watoto wadogo kwa kuwafundisha haki za kibinadamu ambazo ni muhimu, na waweze kujua kumpiga, kumchukia mwenzako ni kosa na vilevile ni vyanzo vya uvunjifu wa amani, huku wakiwafundisha kuwa dini, kabila, rangi kisiwe kigezo cha kuwatofautisha  kwa kuwa binadamu wote ni wamoja kwa haki na usawa, maana wote sisi “we are one Family under God” alisema.

Martha Nghambi alisisitiza kuwa kampeni hii ni endelevu na itakuwa ikiwahusu watoto wadogo na vijana nchini, alisema Martha Nghambi.

Picha zaidi

IMG-20160530-WA0009IMG-20160530-WA0008IMG-20160530-WA0007IMG-20160530-WA0005IMG-20160530-WA0004

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s