Serikali yaanza kutumia TEHAMA Kuendesha mchakato wa Ajira katika Utumishi wa Umma.

Serikali imeanza kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ( TEHAMA) katika kutangaza nafasi za kazi,kupokea maombi,kuwaita waombaji kazi kwenye usaili na kuwawezesha kutumia teknolojia hiyo kupata ajira.
1
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es salaam na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini toka Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira Bi Riziki Abraham wakati wa mkutano na Vyombo vya Habari uliolenga kueleza mikakati ya Serikali kuboresha mfumo wa kupokea maombi ya ajira  na kuyashughulikia.

“Sekretarieti ya Ajira inatoa rai kwa waombaji fursa za Ajira kujisajili katika mfumo wa Ajira unaopatikana kupitia anuani ya tovuti ya http://www.ajira.go.tz na mfumo wa” job alert system” au kupitia simu za kiganjani kwa kupiga 15200# ili kuomba fursa za ajira zinazopatikana Alisisitiza Riziki.

Akifafanua kuhusu faida za kutumia TEHAMA kuendesha mchakato wa ajira, Riziki amesema kuwa mfumo huo unasaidia kupunguza idadi ya siku za kuendesha mchakato wa ajira kutoka siku 90 hadi 52 kwa sasa.

Aliongeza faida nyingine kuwa ni Serikali inapanua wigo wa utoaji taarifa za uwepo wa fursa za Ajira hasa kwa waombaji wa ajira waishio vijijini.

Alisema mfumo huu unalenga kupunguza changamoto kadhaa zikiwemo malalamiko ya baadhi ya waombaji fursa za ajira kuhusu upotevu wa maombi yao ya kazi.
Hadi kufikia Mei, 2016 jumla ya waombaji wa fursa za Ajira waliokuwa wamejiandikisha kwenye mfumo wa utumaji maombi ya kazi walikuwa (97,765).

Aidha jumla ya waombaji wa fursa za Ajira 89,484 wamejiunga kwenye mfumo wa kupata taarifa za uwepo wa fursa za Ajira kupitia simu za kiganjani.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s