Sina chuki na Simba-Jerry Muro

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha klabu ya Yanga, Jerry Muro amesema wanaoamini kuwa ana chuki na uongozi wa klabu au mashabiki wa Simba wanajidanganya.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha klabu ya Yanga, Jerry Muro.

Muro amesema hayo siku moja tu baada ya kuhudhuria mazishi ya kiongozi wa zamani wa Simba, Said Pamba.

 

Muro alijumuika na wanachama na mashabiki wa Simba, akiwemo mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo, Hassan Dalali na Rais wa sasa, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’.

“Nilisisitiza toka mwanzo kuwa kuna maisha baada ya soka, kumbuka Yanga na Simba ni watani, kwenye utani wakati mwingine kuna maneno ya maudhi”

Aidha, Muro amesema hajawahi kuwa na chuki na Simba, lakini anataka Yanga ifanikiwe kwa kuwa yeye ni Yanga hata kabla ya kuwa kiongozi. Pia ameongeza kuwa ataendelea kuipigania klabu yake ya Yanga.

Jerry Muro amekuwa akionyesha kujiamini na kuwachanganya watu wa Simba kwa maneno yake ya kejeli ikiwa ni pamoja na kuwatungia majina ambayo yamekuwa maarufu.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s