Mary Rusimbi: jamii isidharau uongozi kwa wanawake

Jamii ya kitanzania imeombwa kutodharau suala la uongozi kwa wanawake huku wanawake wenyewe wameombwa kuungana na kuwa kitu kimoja ili waweze kuwa sehemu muhimu ya kupelekea kuondoa matatizo yaliyopo katika jamii kwa kushiriki katika masuala mbalimbali ikiwamo siasa na uongozi.

Mary Rusimbi mkurugenzi wa Women Fund Tanzania (picha na maktaba)

Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa shirika la Women Fund Tanzania Mary Rusimbi wakati wa kongamano la wanawake ,katiba na uchaguzi lililoandaliwa na mtandao wa wanawake nchini lenye lengo la kujadili fursa ,changamo,pamoja na matazamio ya nafasi ya ubunge wa viti maalumu nchini.

Naye mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo Anna Mghwira ambaye alikuwa mgombea Rais pee mwakanamke katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana alisema vitendo hivyo vinasababishwa na wanawake wenyewe kutokujiamini pindi wanapoomba nafasi za kugombea na kutegemea msaada kutoka kwa wanaume licha ya wenyewe kuwa na uwezo wa kusimama mwenyewe. Hivyo wanawake washiriki kuijenga

Kwa upande wake mratibu wa taifa TWCP-Ulingo dr. Ave Maria Semakafu amevitaka vyama kubadili mfumo wa sasa wakuwapata wabunge wa viti maalumu pamoja na kuitaka jamii kubadili fikra za kila mwanamke aliyefanikiwa kuwa amewetumia rishwa ya ngono kupata nafasi hiyo.

Aidha wamesema rushwa ya ngono haitaisha nchini kutokana na wanawake kupenda watu wenye vitu pamoja na wanawake wengi kutojiamini katika kushughuli zao.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s