BIASHARA YA UJAMBAZI HAILIPI:KAMISHINA SIRRO.

Jeshi la polisi kanda maalumu  ya Dar es salaam linamshikilia mtu mmoja kwa tuhuma za kuhusika na matukio mbali mbali ikiwemo ya  ujambazi  jijini hapa.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kamishina wa polisi kanda maalumu ya dar es salaam,Simon Sirro  amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa EUJI  ELIAS mwenye umri wa miaka 38 mkazi wa yombo duvya Temeke baada ya watu wasiojulikana kuvamia kampuni ya Group six na kumjeruhi muhasibu wa kampuni hiyo nakufanikiwa kupora magari mawili;vipande 13 vya meno ya tembo pamoja na mashine ya kukatia vyuma.

Katika hatua nyingine kikosi maalumu cha kupambana na majambazi kimemuua kwa kumpiga risasi mtu mmoja ambaye jina lake halijajulikana  katika eneo la masaki jijini humo baada ya kutaka   kumvamia  mwendesha bajaji  na kutaka kumpora , ambapo jehi hilo lililfika  katika eneo la tukio na kufanikiwa kumkamata jambazi huyo.


Aidha jeshi hilo limewataka wakazi wa jiji la dar es salaam kuendelea kuwafichua waharifu mbalimbali wakiwemo wanaomiliki silaa kinyume cha sheria ili kuuhakikisha wanapambana na  vitendo viovu hapa nchini.

 

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s