Muitikio wa uchangiaji damu ni mkubwa Dar es salaam

Dar Es Salaam. Mwitikio wa jamii katika uchangiaji wa damu unaendelea kuwa mzuri siku hadi siku kutokana na elimu ya uhamasishaji inayotolewa na Mpango wa taifa wa damu salama na wadau wengine wa masuala ya afya.

news 1

Hayo yalisemwa jana na Afisa mhamasishaji jamii wa Damu salama kanda ya mashariki Mariam Juma wakati wa tukio la kuchangia damu lililofanywa na kikundi cha ‘Indian Community’.

“Bajeti ya damu mwaka 2016/2017 kulingana na tafiti tulizozifanya mahitaji ya damu ni chupa 230,000 mwitikio wa jamii ni mzuri na tumejipanga kuendelea na utoaji wa elimu na kufanya hamasa katika taasisi mbali mbali ili kufikia lengo”, alisema Juma.

news 1

Naye Mwenyekiti wa ‘Indian Community’ Dkt Sathendra Kasahla alisema lengo la kufanya tukio hio ni kuonesha jamii nzima kama uchangiaji wa damu ni mhimu kwani watu wote ni wahitaji wakati wowote wasioufahamu.

“Watu kila siku wanapata ajari huenda kesho ni wewe au mimi wake zetu na dada zetu wanajifungua wakihitaji damu kama hatukutoa sisi mapema itapatikana wapi wakati hakuna maabara yoyote duniani inayotengeneza damu”, alisema Kasahla.

news3

Naye Manoi Kumor ambaye ni mmoja ya watu waliokuwa wakichangia damu alisema Jamii inapaswa kuwa na utaratibu wa kudumu wa kujitolea damu kwani ni kitendo mhimu ambacho huokoa maisha ya watu.

“Kuchangia damu ungekuwa ni uataratibu wa kila siku kwa kila raia basi kusingekuwepo na tatizo la upungufu wa damu katika hosipatli zetu”, alisema Kumor

 

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s