Global Peace Foundation Tanzania: wazazi jengeni mahusiano mazuri kuleta amani.

Wazazi wa kitanzania wametakiwa kujenga misingi malezi bora ya malezi ili kuleta amani ndani na nje ya familia.

img_1306

Akizungumza mapema leo katika mjadala ambao umefanyika katika zahanati ya Tandale jijini Dar es salaam mkurugenzi mkazi wa Global Peace Foundation Tanzania Martha Nghambi amesema kuwa wazazi ni lazima washiriki kikamilifu katika kujenga misingi ya malezi.

img_1266

Mjadala huo uliudhuriwa na watu mbalimbali waishio tandale na manzese na sehemu zingine za dar es salaam wakiwemo wenyeji ambao ni Tandale Youth Development Center, wadau wengine ni wawakilishi kutoka Youth of United Nations Association, (YUNA), GIDA na wengineo.

fb_img_1476639418980

Naye mwanaharakati wa mmoja kati ya wanaharakati kutoka TYDC Loveness Msuya aliongeza kwamba vijana wa kike wanatakiwa kujitambua na kusimamia ndoto zao ili waweze kufanikiwa kwa sababu wimbi la vijana wengi hukimbilia mambo ambayo hayako katika malengo yao.

img_1333

Huku Martha Nghambi akiongeza kuwa kuharibika kwa vijana wengi kimaadili ni kutokana kukosa mahusiano ya karibu kati ya wazazi na watoto wao sababu hiyo hupelekea kukosekana kwa amani ndani ya familia.

img_1311

Hivyo ametoa rai kwa vijana na wazazi kuungana kwa pamoja ili kuleta jamii iliyobora yenye amani na upendo kwa kuwa bila ya hivyo nchi yaweza kukosa amani.

Baadhi ya vijana ambao walishiriki katika mjadala huo walisukumiza lawama kwa wazazi huku wakisema kuwa chanzo cha watoto wengi wa kike kushindwa kutimiza malengo yao yanapelekea na wazazi kukosa kuwasimamia vyema sababu ambayo wengi hupelekea kupata mimba za utotoni na hata wakati mwingine kuolewa mapema na kukatiza ndoto zao.

img-20161016-wa0000

Baadhi ya wazazi ambao pia walishiriki wameomba wazazi kuwasimamia watoto kuanzia nyumbani hadi shule ili kuweza kuwapa ulinzi wa kutosha, pia wakitupia lawama za maendeleo ya teknolojia ambayo hufanya vijana wengi kuharibikiwa na kujiunga na makundi rika.

img_1226

Tanzania Global Peace Foundation imeitaka jamii ya watoto wa kike wametakiwa watengeneze ndoto na malengo ili kuwawezesha kujitambua na kuachana na makundi rika, nao wazazi wametakiwa kuwa na mahusiano ya karibu pamoja na watoto ili kuleta amani.

img_1304

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s