VIJANA WAUZA TAMTHILIA NA FILAMU ZA NJE WAANDAMANA KUIOMBA SERIKALI KUWARUHUSU WAUZE CD HIZO.

WAFANYABIASHARA wadogo wadogo ‘Machinga’ wanaouza filamu za kigeni wameandamana wakiomba kukutana na Rais Dr John Magufuli ili kusikilizwa juu ya kupigwa marufuku kuuza filamu hizo hapa nchini.

Marufuku hiyo ilitolewa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Harrison Mwakyembe, siku chache baada ya kuteuliwa katika nafasi hiyo mara baada ya kukutana na waigizaji wa ndani ambapo walieleza malalamiko yao juu ya filamu za nje kuharibu soko la kazi zao.

Wamachinga hao waliandamana jijini Dar es Salaam jana katika soko la Kariakoo katika Mtaa wa Aggrey ambako  kuna maduka wanakoenda kuchukua mikanda ya filamu za nje ‘CD’ na kusambaza mtaani huku wengine wakiweka katika vibanda kwa ajili ya kukodishia wateja wanaohitaji.

Wakizungumza na waandishi wa habari wafanyabiashara hao walisema Waziri huyo alitoa maamuzi hayo kwa kusikiliza upande mmoja ambao ni walalamikaji bila kuwapa nafasi ya kujieleza jambo ambalo wanalipinga.

Mmoja wa machinga hao Hanzuruni Mohamed alisema aliyekuwa Waziri katika Wizara hiyo Nape Nnauye alikuwa akisikiliza pande zote kabla kufanya maamuzi na kuongeza kwamba walishakaa vikao mbalimbali kwa ajili kutafuta mwafaka lakini Mwakyembe ameshindwa kufanya hivyo.

“Nape alikuwa anafanya maamuzi kwa kufuata pande zote mbili, huyu katoa siku 10 tu kufungia filamu za nje, hapa kuna vijana zaidi 1000 fikiria tutafanya kazi gani, tukiwa panya road nchi itakuwaje tunakuomba Rais uliangalie hili sisi ni vijana wako” alisema Mohamed.

Naye Halima Bakari alisema kufungwa kwa biashara hiyo kutamwathiri maisha yake kwani alikuwa akitegemea biashara ya filamu kuendesha maisha yake na kuhudumia familia yake na kusema awali alikuwa akifanya biashara ya kujiuza biashara aliyoiacha baada ya kujiingiza katika soko la filamu.

“Mwanzo nilikuwa najiuza nategemewa na mdogo wangu yatima, sasa hivi mabosi wamefunga maduka wakisema wanaogopa kufungwa kutokana na kauli ya Waziri, sasa hivi hatuna ajira nyingine mimi ni binti bila kutoa penzi sipati kazi na kauli mbiu ni Hapa kazi tu, Rais tusaidie tutaenda wapi” alisema Bakari.

Kwa uapnde wake Maliky Ally alisema wametii kuacha kuuza filamu lakini wamaomba kusikilizwa upya ili kuwe na makubaliano yatakayohusisha pande zote kwasababu hiyo ni ajira wanaoitegemea kuendesha maisha yao.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s