Global Peace Foundation Tanzania: Vijana baada ya shule waepuke uvunjifu wa amani.

Taasisi ya Global peace Foundation Tanzania imewataka vijana wa kitanzania kushiriki katika kulijenga taifa pindi wanapohitimu masomo yao wakiwa shule na vyuoni ili kuepuka kujiingiza katika matukio ya uvunjifu wa amani.

Global peace Foundation Tanzania  wakiendeleza mfululizo wa warsha zao za kuwajenga vijana leo wakishirikiana na kituo cha vijana wa Tandale Youth Development Centre (TYDC)  kimeendelea kutoa warsha kwa kuwapa elimu vijana ya maisha baada ya shule.

Kamala Dickson mwanaharakati wa masuala ya vijana kutoka Global peace Foundation Tanzania amewataka vijana kuwa na mawazo chanya wakati wanapokuwa mashuleni, sababu vyanzo vya vijana kujiingiza katika matukio ya uvunjifu wa amani ikiwamo kujiingiza katika makundi ya kigaidi.

“Vijana wengi wakihitimu masomo yao wanakosa kujitambua kutokana na ugumu wa maisha uliopo hivyo kupelekea kuweza kushawishika na vikundi vya uvunjifu wa amani” Alisema.

Mmoja wa vijana ambao waliiudhuria katika mdahalo huo Mohamed Jafari alisema wanafunzi wakaiwa mashuleni fikra zao zainajengwa katika kuajiriwa pia kuchagua shughuli za kufanywa, “Vijana wanatakiwa wajamiiane na mazingira ya kawaida na wafanye shughuli mbalimbali”. Alisema.

Tatizo la vijana kukosa jaira ni janga la kimataifa nchi nyingi zimekuwa zikikumbwa na lawama kutoka kwa serikali kushindwa kuwaandalia ajira vijana wengi wanaomaliza shule na vyuo.

Wengi wa wachangiaji walisema vijana wanatakiwa wajitambue, wasiwe wa binafsi na ubunifu, na kuondokana na akili za wengi zimeadumazwa fikra zao, na kukimbilia mijini.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s