Timbulo awataka wasanii wasimlilie

Mwanamuziki anayetamba na ngoma ya ‘Mshumaa’, Timbulo amewataka wasanii wasipate presha kipindi hiki ambacho yeye anaachia ngoma mara kwa mara kwani alikaa nje ya ‘game’ muda mrefu hivyo sasa anafanya kazi kwa bidii ili kwenda sawa na waliopo sokoni.

Akizungumza kwenye 5Selekt ya EATV , Timbulo amesema kwamba yeye ni mfuasi wa muda hivyo kipindi alichokuwa amekaa kimya wasanii wengine walikuja na kufanya vizuri hivyo sasa ni muda wake kuwaonyesha uwezo wake lakini wameanza kuogopa na kulalamika.

“Sasa hivi nimeamua kutoa vyuma ili niende sawa na wenzangu waliokuwepo kwenye game, kuna baadhi ya wasanii mpaka wanalia wananiambia mbona sasa unazidisha kila siku wewe tu unaachia ngoma mpya, nawaambia tulieni nataka tuende sawa maana wao wameshaniacha mbali sitakiwi tena kutembea.

Kwa upande mwingine Timbulo amesema kwamba hafahamu ukubwa alionao Tanzania kwani bado anajiona hajafika mahali ndio maana anakaza kupambana kila siku

“Mimi sijui ukubwa wa jina langu, watu wa nje huko ndio wanafahamu nina ukubwa gani. Watu wanapohoji umri niliokuwepo kwenye game na ukubwa wa jina langu mimi nitawajibu na deserve kuwa hivi kwani mimi nilikaa kimya muda mrefu nikawaacha wengine wafanye, lakini namshukuru Mungu bado watanzania wananipa sapoti ya kutosha”. Aliongeza.

Pamoja na hayo Timbulo amesema anaamini huu ndio muda wake sahihi wa kung’aa ingawa alikuwa kimya muda mrefu kwenye ‘game’.

“Mimi ni muasisi mzuri wa muda, kung’aa kwangu siyo kwamba nimebadilisha uongozi, waliokuwa wakinisimamia toka naanza muziki ndio mpaka saivi nipo nao ingawa wapo wasanii kibao walioondoka na kutukana kwamba management haina pesa. Hivyo sasa hivi kuonekana nafanya poa ni kwa sababu muda wangu umefika wa kung’aa”, T imbulo alisema

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s