Global peace foundation Tanzania: kumpa wanawake elimu bora ni kujenga jamii bora.

Katika kuelekea siku ya wanawake duniani Global Peace Foundation Tanzania wameendelea kampeni yao ya kuhamasisha amani duniani ambapo siku ya leo walikuwa wakiadhimisha siku hiyo katika shule ya sekondary ya St. Anne Marie Accademy ya jijini Dar es salaam.

IMG_0904

katika siku hii ya leo Global peace Foundation wameadhimisha kwa kauli mbiu ya “Kumpa mtoto wa kike elimu bora ni kujenga jamii bora, ambapo iliendeshwa na Global peace foundation chini ya mwakilishi wa Irene Ishengoma na mgemi mwalikwa akiwa ni makamu wa rais wa chuo kikuu cha Dar es salaam Anastasia Anthony.

IMG_1085
Mwakilishi kutoka Global Peace Fondation Women Irene Ishengoma katikati. amabye leo alikuwa mzungumzaji mkuu na msimamizi wa Hafla ya kushehekea siku ya mtoto wa kike.

Akizungumza katika afhla hiyo Irene alisema kuwa Global peace foundation tanzania inaamini kuwa mwanamke ni chachu ya amani katika taifa “Mwnamke ni kiungo imara katika familia sababu mwanamke amekuwa mstari wa mbele katika utunzaji wa familia basi vivyo hivyo katika utunzaji wa amani.

ameongeza kusema kuwa hadi watotot wameweza kuja shuleni ni kutokana na amani iliyokuwepo katika taifa la Tanzania basi shime tuitunze amani sababau zipo nchi nyingi duniani ambazo wakati huu wanaisaka amani huku akiitaja nchi ya syria kuwa ni miongoni mwa nchi ambazo zinaisaka amani wakati huu.

aidha amewataka wazazi walezi pamoja na walimu kushirikiana katika kuwapa elimu watoto wa kike kwa manufaa ya taifa. “wazazi na walimu wasiache watoto wakipotea wawapatie elimu ya kujitambua na kujithamini pia”. Alisema.

Huku makamu wa Rais katika chuo kikuu cha dar es salaam  (UDSM) Anastasia Anthony siku hii ya wanawake ameitaka jamii ya watoto wa kike kujitambua kujitahmini na sababu wanawake ni nguzo kubwa katika jamii, mashuleni, vyuoni hata majumbani, “walioko vyuoni na mashuleni ikiwa leo tunasherehekea siku ya mtoto wa kike watambue baada ya muda mchache watakuwa wanawake moja kwa moja.

IMG_1087
Anastasia Anthony makamu wa Rais wa chuo kikuu cha Dra es salaam (UDSM), mapema leo akiwa katika shule ya ST> Anne Marie katika kuelekea kilele cha siku ya mtoto duniani.

Kila ifikapo tarehe 8 mwezi machi kila mwaka dunia inaadhimisha siku ya mtoto wa kike duniani. ambapo taasisi ya global peace foundation imeadhimisha siku ya leo kuelekea kilele cha siku hiyo katika shule ya ST. Anne Marie kwa kujumuika na watoto wa kike kuwapa elimu na michezo pamoja na burudani.

Picha na matukio mengine…

IMG_0895IMG_0902IMG_0945IMG_0955IMG_0975IMG_0977IMG_1027IMG_1032IMG_1035IMG_1036IMG_1038IMG_1042IMG_1078IMG_1081IMG_1083

IMG_0987IMG_1058IMG_1075IMG_1080IMG_1101IMG_1102IMG_1103IMG_1104

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s