Sevilla wavunja mwiko wa miaka 60

Baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Manchester United klabu ya Sevilla imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali kwa mara ya kwanza tangu ifanye hivyo mara ya mwisho miaka 60 iliyopita.

Sevilla ambao ni mabingwa wa historia wa kombe la Europa League, walifanikiwa kupata ushindi huo kwenye uwanja wa Old Trafford mara baada ya timu hizo kutoka suluhu ya 0-0 kwenye uwanja wa Sanchez Ramon Pizjuan wiki mbili zilizopita.

Mabao ya Sevilla yalifungwa na mshambuliaji Wissam Ben Yedder, aliyeingia kipindi cha pili akichukua nafasi ya Luis Muriel dakika 72 na kufunga ambao hayo ndani ya dakika 5 akianza dakika ya 74 na kumaliza dakika ya 78.

Bao pekee la Manchester United lilifungwa na Romelo Lukaku dakika ya 84 lakini halikuisaidia timu hiyo ambayo ni bingwa wa UEFA mara tatu. Man United sasa imebaki ikiwania kikombe cha FA kutokana na mbio za ubingwa wa EPL kutawaliwa na Man City.

Baada ya mchezo huo, Ben Yedder alitangazwa kuwa mchezaji bora wa mchezo (Man of the Match). Sevilla kwasasa inashika nafasi ya 5 kwenye msimamo wa La Liga huku Man United ikishika nafasi ya 2 kwenye msimamo wa EPL.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s