Chelsea Kumkosa Courtois?

Klabu ya soka ya Chelsea kuelekea mchezo wake wa ligi kuu ya England dhidi ya Tottenham, huenda ikamkosa mlinda mlango wake namba moja Thibaut Courtois baada ya kuumia akiwa na timu ya taifa ya Ubelgiji.

Mchezaji huyo amelazimika kuondolewa kwenye kikosi cha Ubelgiji kitakachokabiliana na Saudi Arabia siku ya Jumanne Machi 27 kwenye mechi ya kirafiki ya kalenda ya FIFA kwa mwezi Machi.

Kabla ya Courtois kuumia kocha wa Chelsea Antonio Conte hivi karibuni alithibitisha kuwa nyota huyo anasumbuliwa na misuli, tatizo ambalo lilianza baada ya mchezo wa robo fainali ya kombe la FA.

Nafasi ya Coutois kwenye mchezo huo inatarajiwa kuzibwa na Simon Mignolet wa Liverpool au Koo Casteels na Matz Sels ambao ndio chaguo jingine ndani ya kikosi hicho cha kocha  Roberto  Martinez.

Chelsea itakuwa nyumbani kucheza na Tottenham Jumapili ijayo. Chelsea tayari inashika nafasi ya 5 kwenye msimamo wa ligi wakiwa na 56 huku Tottenham wakiwa katika nafasi ya 4 wakiwa na alama 61.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s