Tunahitaji ubingwa wa Ulaya – Guardiola

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola ameweka wazi kuwa klabu hiyo inahitaji taji la Ulaya kutokana na uwekezaji ambao umefanyika katika kioindi cha mika 10 na tayari umeleta mafanikio kwenye ligi ya ndani.

“Tunahitaji mataji ya Ulaya japo ni jambo gumu lakini tunalitarajia iwe msimu huu au msimu ujao lakini mapema tu tunahitaji kutwaa taji hilo”, amesema Guardiola kwenye mkutano na wanahabari kuelekea mchezo wa marudiano kesho dhidi ya Liverpool.

Akiongelea kuhusu uwezekano wa kupindua matokeo ya mechi ya kwanza ambapo walipoteza kwa mabao 3-0 ugenini, Pep amesema kila kitu kinawezakana ndio akitumia mfano wa walichofanya Barcelona msimu uliopita walipopindua 4-0 na kushinda 6-1 dhidi ya PSG.

Aidha Guardiola amesema kuwa najua wazi timu yake inahukumiwa kwa matokeo ya hivi karibuni lakini yeye kama kocha ana furaha na kiwango cha timu yake na anaamini kuwa ndio timu yenye kiwango kizuri kwasasa.

Manchester City kesho watakuwa wenyeji wa Liverpool kwenye mchezo wa marejeano kwenye ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo matajiri hao wanahitaji kushinda kuanzia mabao 4 huku wakiwa hawajaruhusu wavu wao kuguswa.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s