Kiama cha makocha wa VPL chaanza

Ikiwa ni takribani siku mbili tangu aliyekuwa kocha wa Yanga Mzambia George Lwandamina, aachane na klabu hiyo na kurejea kwenye timu yake ya zamani Zesco United, Mbao FC nayo imemfuta kazi kocha wake Etienne Ndairagije.

Taarifa ya Mbao FC imeeleza kuwa klabu hiyo imeachana na kocha huyo ambaye ni raia wa Burundi na nafasi yake imechukuliwa na kocha mzawa Fulgence Novatus. Novatus atakuwa na kibarua cha kuinusuru timu hiyo katika hatari ya kushuka daraja.

Novatus ni kocha mzoefu ambaye amewahi kufundisha timu za Toto Africans, Singida United pamoja na timu ya taifa (Taifa Stars), katika vipindi tofauti. Mbao FC kwasasa inashika nafasi ya tatu kutoka mwisho ikiwa na alama 23 katika mechi zake 24.

Kwa upande mwingine tetesi kubwa zilizopo ni kuwa klabu ya soka ya Azam FC imepanga kuachana na kocha wake raia wa Romania Aristica Cioaba huku ikidaiwa mipango ya kumnasa kocha wa Singida United Hans Van Pluijm ili achukue mikoba ya Cioaba inaendelea.

Azam FC kwasasa inashika nafasi ya tatu nyuma ya Simba na Yanga ikiwa na alama 45 ambazo ni alama 2 chini ya Yanga yenye alama 47 katika nafasi ya pili na alama 10 chini ya Simba yenye alama 55 kileleni.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s