Nandy aomba radhi mpaka kwa kanisa

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nandy ambaye hi leo amekutwa na balaa la kuvuja kwa video yake ya utupu, ameomba radhi kwa watu mbali mbali ikiwemo kanisa lake juu ya video hiyo, inayomuonyesha akiwa faragha na msanii mwenzake Bill Nas.

Akizungumza hilo Nandy amesema video hiyo ni ya mwaka 2016, na haelewi kwa nini mtu aliyeivujisha kaamua kufanya hivyo, lakini ni kitendo kilichomuumiza sana hivyo anaomba msamaha kwa jamii, mashabiki, kanisa na kila mtu ambaye imemgusa kwa namna moja au nyingine wamsamehe, kwani tayari anajutia jambo hilo.

“Nimesikitika sana, hiyo video ni ya ukweli ni ya mwaka 2016, nilikuwa na mahusiano na Bill Nas na tulikubaliana iwe siri, sasa sielewi kwa sababu gani kaamua kuvujisha, nimesikitishwa sana, ni video ambayo ilishutiwa kwa snapchat, sasa sielewi wakati ameipata hiyo video alikuwa nayo au alichukua mwenyewe, sijui niseme nini, naomba radhi sana kwa familia yangu, kanisani kwangu, serikali yangu, mashabiki, naomba radhi sana, adhabu ya maumivu ambayo nayapata imetokana na kumuamini mtu, ilikuwa ni private”, amesema Nandy.

Wawili hawa mara kwa mara walikuwa na skendo ya kuwa na mahusiano lakini wamekuwa wakikanusha, na watu kuanza kuibua hisia upya baada ya Nandy kumtakia heri ya siku ya kuzaliwa Bill Nas kwa kupost picha inayomuonyesha akiwa kifuani kwake.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s